Friday, October 31, 2008

A BOYS

Wakwanza kushoto ni (JACO B) mwengine huyo kulia ni (BAD SKY) kwa pamoja wanaunda kundi la (A BOYS) wakiwa pamoja na (JAY I)

KARIBU ZANZIBAR MAMA


Kwahabari tulizo kuwa nazo kwamba mwana muziki huyu anaitwa (CIARA)
anatarajiwa kuwasili katika visiwa vya (ZANZIBAR) hivi karibuni wadau mpo
tayari kumpokea?

SHOW ZENYE MIZUKA


Mashabiki wa hip hop wakiwa wamepanda mizuka wakimsogelea karibu mwana muziki mkali wa hip hop ( ZANZIBAR) anaitwa (RICO SINGLE)

WASANII WANAPO KUTANA


Hao wana dada wanaitwa (UNIQ DADAS) wakiwa pamoja na (RICO SINGLE) ndani ya studio za (JUPITER RECORDS ZANZIBAR)

SANDRA


MAMBO VIPI WADAU?
huyu ndie sandra a.k.a bint kiziwi
huyu huyu mwana dada alipiga
video ya kwanza na (KASSIM) inaitwa
haiwezekani lakini imewezekana kwa (ZE DANTONI)
kupiga nae video ya bint kiziwi halafu kufunga nae ndowa kabisa. hongera dada.

ZIFF LIVE SHOW


(Rico single) akiwa na (Armstrong dady) katka tamasha la (ZIFF ZANZIBAR)
wazeiyaa wakipiga makamuzi kimtindo

AKHENATO NA DJ SIDE


(DJ SIDE) akiwa pamoja na producer (LIL GHETO) pamoja na (DOT COM) na mwana dada (SWEETY RAY) katika studio za (AKHENATO RECORDS )

SNAR LEE NA RICO SINGLE


Vichwa 2 vyote kutoka zenji hao nio wakali wa ukweli kivyovyote kwenye gemu ya music wa bongo flava kwasasa (SNAR LEE) inasemekana anaishi
ulaya katika nchi ya (HOLAND) mzuka kaka

AMINA CHENGO


Hapo ndo utapo juwa umuhimu wa huyu dada wadau wengi na mashabiki wa (ZENJI FM RADIO)
wamekuwa wakijiuliza maswali mengi sana kuhusu
(AMINA CHENGO) wanadai wame mmiss sana tena sana siku hizi hasikiki kwenye radio lakini inadaiwa kwamba bado yupo (ZENJI FM RADIO) je kama yupo mbona hatumsikiii? WAHUSIKA tupeni issue zake yuko wapi huyu?

WAZE FEIYAA


(BANDAGO HAULE) akiwa na producer wa (JUPITER RECORDS ZANZIBAR) anaitwa (LABIZO MZUNGU) wanananchi wa (ZANZIBAR) wanaulizana huyu jamaa ( BANDAGO) kwa sasa
amekimbilia wapi? tuna tafuta skendo zake tuta wapatia wadau mtajuwa yuko wapi huyu kijana tuombe uzima tuu.

UJIO MPYA


Watakao kuja kuisumbuwa mikaka inayo bana puwa katika uimbaji wa music wa bongo flava ni hawa hapa. vijana 2 kushoto anaitwa (SULTANI)
na kulia anaitwa (ABDULL) vijana hao ni wakali wa kikweli kweli sio siri hawa ni vipaji kutoka mbinguni kweli.ila kwa sasa wapo katika maandalizi na mafichoni na kusimamiwa na( JUPITER RECORDS ZANZIBAR) wadau ipo siku mtakubali mi sina mengi ni hayo tuu.

MZEE WA KUGENGESHA


Huyu ndiye yule mzee wa kugengesha ngoma za ukweli ukweli yani ngoma za town anaitwa (DJ SIDE) akiwa ndani ya maeneo yake ya makamuzi (ZENJI FM RADIO ZANZIBAR)

SUMA LEE MZEE WA GLASS

Watu wengi wanajiuliza huyu jamaa yuko wapi? majibu hawana wengine waliwahi kusema kwamba kahamia (ZANZIBAR) kumbe si hivyo bali jamaaa (ZANZIBAR)
alikuja kurecords song yake moja tu ambayo ilifanyiwa na video yake pia ndani ya kampuni ya (JUPITER RECORDS ZANZIBAR ) nyimbo ilikuwa inaitwa (ASALI) kwasasa jamaa haonekani
hatujuwi yuko wapi? wadau anae juwa taarifa zake atutumie kupitia eimail yetu hiyo hapo juu.

BI KIDUDE NA WAJUKUU


Wanao onekana hapo ni wadau wa music wa asilia na music wa kizazi kipya
tukianzia mkono wa kushoto (FID Q) anafuatia (BI KIDUDE) mzazi wa wazazi (HASS T) na producer ( DUCHI) na nyuma kabisa ni producer (LABI ONE) kwa pamoja wakiwa katika studio za jupiter records (ZANZIBAR)

MKALI WA LEO


WADAU MAMBO VIPI? huyo hapo ndiye dada mkali wa leo huyu dada anaitwa (GRACE) anapatikana maeneo ya 96.8 (ZENJI FM) sauti ya pwani mjini (ZANZIBAR) huyo dada alikuwa anapiga show ya kipindi cha rege kinacho ruka hewani siku za jumapili saa 3 usiku hadi majogooo. kwasasa huyu dada simsikii tena wadau
wameomba kujuwa yuko wapi kwa sasa? mwenye habari zake tunaomba atutu mie kupitia eimail yetu hiyo hapo juu. kila la kheri ..

MKALI WA KUWARUSHA


(RICO SINGLE) akiwa rusha mashabiki wake wa music wa kizazi kipya yani bongo flava ndani ya ukumbi maarufu mjini (ZANZIBAR) ukumbiwa (JIMKANA CLUB ZANZIBAR) picha na matukio yote mzuka sana.

MOJA YA KAZI ZA ARMSTRONG DADY


Hiyo picha waungwana anaonekana
kassim mganga akiwa na sandra wa binti kiziwi wakiwa katika mwendo
huku wakiwa wanapigwa picha za
clip za video ya kasimu haiwezekani
nyimbo ya mwanzo ya kassim mganga video hiyo ikiwa inafanywa
na chief editor wa jupiter videos zanzibar bwana (Armstrong dady)
katika kisiwa cha changuu zanzibar.

Thursday, October 30, 2008

DJ SIDE WA ZENJI FM


Mwana kaka wa town huyoo. anaitwa (DJ SIDE) kutoka (ZENJI FM RADIO)
96.8 sauti ya pwani mjini (ZANZIBAR) akiwa katika moja ya show yake ya ukweli ukweli
kipindi marufu kabisa mjini zenji kinacho kimbiza mbayaa mitaani kinaitwa za crush
kinacho ruka mida ya saa 8 mchana mpaka saa 10 jioni hapo utapata kusikia mahabari ya
ukweli ukweli ya intertaiment na maburudani mengi. ni hayo tu mzeiyaaa

LIL GHETO

WADAU mambo vipi? huyo ndie (LIL GHETO) ni producer wa STUDIO za
(AKHENATO ) ambazo kwa sasa zimehamishiwa mjini daresalam na kuu ngana na uswazi
records chini ya usimamizi wa adam juma wa virtual lab.

JUPITER RECORDS IPO HUMU


Wadau hili jengo ndilo jengo lenye kituo cha radio inayo tamba visiwani zanzibar katika media zote na sinyengine bali ni (100.9 ) coconut fm zanzibar lakini pia usisahau kwamba jengo hili
ndio inapo patikana studio za jupiter records zanzibar khorofa ya kwanza ipo studio hiyo,
watu wote mnakaribishwa radio na studio karibuni wadau wote.

MWANA DAFADA


Mwana dada huyu inasemekana ndie mwana dada mwenye mvuto wa
kimapenzi kuliko wanawake wengi wa mjini. mimi sijuwi lolote kuhusu
hilo lakini wewe mdau unakaribishwa kutowa comment zako kuhusu hili. ok
ni hayo tuu.

KISIWANI CHANGUU ZANZIBAR


Inasemekana kwamba kisiwa cha changuu zanzibar kina kobe wengi halafu wana miaka mingi sana.hiyo picha unayo iyona hapo ni msanii wa zanzibar mkubwa tu anaitwa (Rico single)
alitembelea kisiwa hicho na hapo akiwa anamlisha kobe chakula aina ya kabich imelezwa kwamba huyo kobe anae pewa hilo jani ana miaka 85 hapo alipo lakini kuna kobe hadi wenye
miaka 300 hapo kisiwani. wadau mnakaribishwa kwenda kujionea.

WAKALI WA JUPITER

Wadau mambo vipi? hao hapo ndio wakali wa jupiter records zanzibar kutoka kusho ni
kijana anaitwa (NIZZO 4 SHOW) na kulia jamaa anaitwa (Rico single) wadau vichwa hivyoo
mna semaje?

UGENI WENYE FAIDA


Hapo unapo waona ni wageni kutoka ujerumani wakiwa na kiongozi wao bwana hafidhi suti
kwapa moja wakiwa katika kikao cha kujadili jambo katika ofisi ya bwana armstrong dady
chief editor wa jupiter video zanzibar akiwa yuko makini akisikiliza jambo kutoka kwa mmoja
kati ya wageni wake walo kuja kumtembelea,

MKALI WA DONTAR

Mwana dada (BABY JAY) a.k.a mkali wa dontar kulia
akiwa na rafiki yake wa karibu..............kwenye picha na
pozi za ukweli (BABY JAY) ni mwanamuziki mkali
wa kike (ZANZIBAR) ambae amesha wahi kujinyakulia tuzo
mbili za mwanamuziki bora wa kike zanzibar wa miondoko
ya bongo flava na wimbo bora wa mwaka wa mwanamuziki
chipukizi wa kike. kwasasa anatamb na wimbo wake
mpya akiwa amempa shavu pasha unaitwa (moyo wangu
umechoka)

MKALI WA TAARABU


Hapo kusho ni bibie ( HUSNA B) mkali wa kuichambuwa taarabu ya town akiwakwenye picha
ya pamoja na rafiki yake wa zamani ( SOFIA MJUNGU) ,husna b ni mtangazaji wa kipindi cha
nipe nikupe cha coconut radio kinacho anza asubuhi saa 4 mpaka saa 8 mchana pia anatangaza kipindi cha mambo ya zenji cha kila jumamosi na jumapili hapo utapata burudani zote kali
coconut fm (100.9) zanzibar

JUPITER LOGO


Hiyo ndio nembo ya kampu kubwa ya kutengeneza
music wa audio na video visiwani zanzibar inajulikana
kwa jina la jupiter records zanzibar.

MKALI WA HIP HOP ZANZIBAR


Huyu ndie mkali wa hip hop Zanzibar
jamaa anatokea studio za jupiter records
Zanzibar mchizi anaitwa (Rico single)
jamaa anangoma nyingi sana maarufu
kwa wasikilizaji music Tanzania nzima
kama sikosei east african au duniani
kwa sasa jamaa anatarajia kuachia
ngoma yake mpya inaitwa (acha waongee)
akiwa amempa shavu (baby jay)mdau kaatayari kupokea hiyo kazi ya mkali huyu.

MZAZI WA WAZAZI


Huyu ndie chief wa ma chief anakwenda kwa jina la hass t mkali wa wakali
akiwa katika harakati za kuwa towa vijana wa mjini katika kuhakikisha ana
kuza vipaji vyao vya music wa bongo flava Tanzania hapo akiwa anaelekea katka
eneo moja zuri sana akiwa anakwenda kupiga show ya kipindi chake cha kila week
kinacho itwa pembe tatu kinacho ruka hewani kupitia luninga ya TVZ kila juma nne,

WAZEEIYAA


Wazeiyaa wa town

kushoto ni anaitwa

Armstrong dady katikati ni mwana dada

anaitwa baby jay huyo mwengine

anaitwa rico single wakiwa katika

picha ya pamoja ndani ya studio za

jupiter records zanzibar.

TAIFA LA KESHO


Watoto wakionekana wakiwa na furaha sana baada ya kumaliza kufanya
kipindi cha watoto maarufu kama chei chei kinacho ruka hewani kupitia kituo bora
cha radio (coconut fm ) visiwani zanzibar, kinacho ruka hewani kila siku za weekend jumamosi saa 3 asubuhi hadi saa 6 mchana. mzazi unaweza kumpeleka mtoto wako
kwenda kujumuika na watoto wenzake na kujifunza vitu mbali mbali ni bure tu wala si kwahela.. karibu coconut fm zanzibar migombani mnara wa mbao..

MKALI WA R&B ZANZIBAR


Huyo mwana kaka hapo anaitwa (sultan )kutoka jupiter records zanzibar.kichwa hicho kinatarajia kuachia
ngoma yake mpya itwaayo (leylah) soon mwanzoni mwa mwezi wa 12 ngoma tayari imepingwa audio na video
hivyo mdau katayari kuipokea ngoma hiyo yaukweli.

PRODUCER WA JUPITER RECORDS ZANZIBAR


Labi one a.k.a labizo ndiye producer wa studio kali mjini zanzibar jupiter records zanzibar
huyo ndie mkali wa ngoma za mjini zinazo tamba sasa kama vile (awena) ya kassim
tuongee kidogo ya (rico single)
na ngoma nyingi kali kali tu ,dahh mzee yuko juu kinoma ni hayo tuuu,,

BARABARA YA AIR PORT ZANZIBAR


Mdau mambo vipi?
hiyo ndio barabara kuu zanzibar
kutoka air port kuelekea mjini
kwenye shughuli za siku zote
je mdau unalolote la kuchangia
kuhusu barabara hii? towa
comment zako kupitia hapa.

BOMBA DJ

Hao hapo wadau ni kikosi cha bomba dj ni ma dj
wa kituo cha radio cha fm hapa zanzibar kinacho tamba sana mjini humu kusho ni( DJ dusco dala) katikati ni (DJ A5) na kulia ni (DJ FLASH)
hao ndio wazee wa kusababisha na ngoma za town zau kweli ukweli bomba dj bomba fm 87.5 zanzibar mdau ikamatie hiyoooo,,

USAFIRI WA ZANZIBAR


Mdau akiwa anapata chenji yake badala ya kushuka katika usafiri
wa aina ya daladala akiwa anatokea mjini katita mishe mishe zake, wadau huo ndo usafiri wa abiria zanzibar,